Kiswahili

Sitaogopa mabaya

Kutangaza ujaji wa tafsiri ya kitabu cha mgombea uraisi wa Marekani Emanuel Pastreich

“I Shall Fear No Evil”

Katikati ya kampeni ya uraisi ya 2020, iliyochanganywa na propaganda na sumu ya ufisadi, mgombea mmoja alisonga mbele ili kuonyesha usahihi wa kisayansi uozo ambao umeingia kwenye jamii yetu. Emanuel Pastreich alitangaza kuwa mgombea huru tu ndiye anayeweza kutumikia uraisi kwa kuonyesha kuanguka kwa vyama vya siasa kuwa vyama vya uhalifu vinavyopingana. Anatuwakilisha kwa mpango madhubuti wa kulibadilisha taifa letu kwa njia ya hotuba zinazoeleweka ambazo zinatuhakikishia sisi kama raia wenye uwezo wa kuchukua hatua, na sio kama wapokeaji tu.

Pastreich anakataa kumpa lawama mtu yeyote, au kikundi, lakini anapendekeza kuwa turudi kwenye roho ya Katiba na, kama Frederick Douglass na Abraham Lincoln, gundua misingi ya maadili kwaajili ya utawala bora ambao umezikwa katika kaburi la kina kirefu na kampuni za uhusiano wa umma, benki za uwekezaji, na vikundi vya wanasiasa na wataalamu waliojiteua.

Kitabu hiki kina mfululizo wa hotuba ambazo Emanuel Pastreich alizitoa kama mgombea huru wa uraisi wa Marekani baada ya kutangaza kwake kwa mara ya kwanza kuwa na nia ya kugombea Februari (2020). Alitoa hotuba, alikutana na Wamarekani wenzake, haswa wale ambao wanateseka na matokeo ya uozo mkubwa wa maadili katika nchi yetu. Kwa maoni yao, kwa msaada wao, alianza kuchora ramani nzuri ya Marekani, wakati unaokuja ambao tunaondoka kwenye utamaduni hatari wa utumiaji, unyanyapaa na vita visivyo na mwisho ambavyo vimeliambukiza taifa kama virusi vya kutisha na kukuzwa na vimelea hatari.

Emanuel Pastreich ameibuka zaidi ya miongo miwili iliyopita kama sauti inayoongoza kwa sera nzuri ya Marekani katika diplomasia na usalama kwa mazingatio madhubuti juu ya tabia nchi na anguko la viumbe mbalimbali, athari mbaya ya teknolojia mpya kwa jamii ya wanadamu, malimbikizo makubwa ya utajiri, na mbio za silaha za ulimwenguni.

Pastreich anajitahidi kuibadilisha mila ya ujamaa aliyofuata Franklin D. Roosevelt na Adlai Stevenson katika maandishi yake na katika hotuba zake.

Anadai kuwa matrilioni ambayo walipewa mashirika mwaka jana yarudishwe, muungano kama wa Amazon na Facebook uendeshwe kama mashirika yanayodhibitiwa, na pia mali za mashirika ya mafuta zichukuliwe mara moja, wamiliki na wasimamizi wao washtakiwe kwa jinai ya kuwasilisha taarifa za ulaghai kwa serikali na watu juu ya mabadiliko ya tabia nchi.

Mtaalam wa Asia anayejua vizuri Kikorea, Kijapani na Kichina, Pastreich alianza kazi yake kama profesa katika Chuo Kikuu cha Illinois, Urbana-Champaign mnamo 1998. Hivi sasa anahudumu kama raisi wa Taasisi ya Asia, chombo cha kufikiria kinachojidhatiti katika diplomasia, usalama na teknolojia iliyoko Washington DC, Seoul, Tokyo na Hanoi.

Tafsiri ya kitabu changu kwa Kiswahili, lugha ya zamani ya kibantu, ina umuhimu mkubwa kwa kampeni yangu na kwa mustakabali ujao wa binadamu. Tafsiri ni yetu sisi kwaajili ya mabadiliko.

Tafsiri ya kitabu hiki inamaana kwamba mimi, kama mgombea wa uraisi wa Marekani, ninawasiliana moja kwa moja na watu wa Afrika kwa lugha yao, na kuwakaribisha kuungana nami katika juhudi za kuunda Marekani mpya, na uhusiano mpya kati ya Marekani na mataifa yote ya Afrika, ambayo yanafuata mkataba wa Umoja Wa Mataifa. Uhusiano huu utakuwa wenye usawa wa haki, na inamaana kuwa Marekani inavuka zaidi kwenye muungano wa kiasili ikiwa na mamlaka ya kikoloni, mwisho, na zaidi uhusiano wa unyonyaji na udhalilishaji kati ya Marekani na Afrika ambao umekuwa tangu zama za biashara ya utumwa.

Uhusiano usiofaa katika zama hizi unaonekana kupitia mfumo wa Bretton Woods (kama vile Benki ya Dunia) mfumo ambao ulikuwa na uwezo wa kweli mwanzo, ila umekamatwa na kudhibitiwa na benki za uwekezaji ulimwenguni.

Umekuwa msemo uliopitwa na wakati baina ya wafanyabiashara na wafadhili kusema kwamba Afrika imedharauriwa, kuwa Afrika ni mustakabali wetu ujao. Kiujumla, kwa mawazo hafifu, wapo sahihi

Bali, tumelishwa kwa muda mrefu sana historia ya Afrika, na taswira ya Afrika, ambayo mizizi isiyofaa imetoka kwenye mkutano wa Berlin wa mwaka 1885. Ilikuwa katika Mkutano huu wa Berlin ambapo Jumuiya ya ulaya, waliwehuka na unyonyaji na uharibifu, maradhi ya kiroho ambayo mwisho yalileta jinamizi la Vita Kuu Ya Kwanza Ya Ulimwengu,ambayo Iliichonga Afrika ili itumiwe kwa faida yao.

Tangu wakati huo, wale waliosoma sana katika “mataifa yaliyoendelea” wanaweza kuona kama Afrika ni mahali pa kuchekesha penye ngao za kikabila na vinyago vya ajabu na vya kushangaza kwenye sebule zao, au wanaona kama Afrika ni kitu cha kutumiwa, ndimu ya kuminywa na kutupwa. Afrika kuwa sehemu, ya mbali sana na ambayo haijulikani, hiyo ilikuwa kitu cha kuvutia tu ili kuweza kutumia watu wake kwaajili ya kazi za mishahara midogo, kuweza kutumia rasilimali zake za asili – bila kujali ni uharibifu gani unafanyika wa kimazingira ambayo Waafrika lazima waishi -Na kuwa tunaweza kulima kwaajili ya soko la bidhaa za watumiaji, bidhaa za matumizi ambayo watu hawayahitaji sana na ambazo zinapoteza rasilimali na hali kadhaa, kama simu janja na michezo ya video, hudhoofisha uwezo wa watu kufikiri.

Hii sio Afrika ambayo ninaigeukia kuwa mshirika mpya nayo. Huo sio uhusiano ninao utaka kati ya Marekani na Afrika katika utawala wangu.

Kwanza, tuna mengi ya kujifunza kutoka Afrika, nyumbani kwa wanadamu, nyumbani mwa mamia ya tamaduni mbali mbali. Tunaweza kujifunza juu ya maelewano na asili, kuhusu kilimo endelevu, kuhusu utawala bora na uongozi mzuri kutoka Afrika na kutoka kwenye historia yenu. Niko hapa, kwa unyenyekevu wote, kujifunza kutoka kwenu.

Pili, tunaweza kuanzisha ushirikiano wa watu wa nchi ya Marekani na Afrika, ili wanafunzi wenu wa shule ya msingi waweze kuwasiliana na mwanafunzi wetu wa shule ya msingi, ili walimu, wasanii, waandishi na wazazi wa Marekani na Afrika, wazungumze moja kwa moja. Hakutakuwa na benki za uwekezaji au mashirika ya kimataifa yanayoingilia mazungumzo yetu.

Tatu, tutakuwa na majadiliano sawa na ya kweli, kulingana na njia ya kisayansi, kati ya wataalamu wetu na wataalamu wenu kuhusu siku za mbeleni za dunia yetu ndogo yenye thamani. Ninajua ni jinsi gani mna wasiwasi kuhusu watoto wenu na nina hakika kabisa kwa kuwa pamoja, kuheshimiana na kusikilizana, na kujifunza, hiyo itarudisha taswira ya asili ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa na kuvuka zaidi kwenye mfumo huu wa uharibifu wa uchumi na mfumo wa itikadi unaohusu dhana mbaya ya ukuaji, matumizi, uzalishaji, na ushindani.

Mwanamke ambaye anajua kupika na kusafisha kwa kikombe kilichojaa maji katika nyanda za juu za Afrika ana ujuzi wa kiteknolojia wenye thamani zaidi kuliko kompyuta ya quantum au teknolojia ya semiconductor katika Chuo Kikuu cha Stanford. Tunataka kujifunza kutoka kwake juu ya uendelevu wa siku zijazo.

Tunapotafuta muundo mpya wa kiitikadi kwaajili ya Dunia yetu yenye thamani, nina hakika kuwa itakuwa hekima ya zamani ya Afrika ndiyo itakayotuongoza.

Asante, raia wa heshima wa Afrika, kwa usikivu wenu. Natumaini kukutana nanyi ana kwa ana katika siku zijazo.